Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapongeza hatua ya kuanzishwa kwa makazi ya mpito ya wakimbizi Libya

Kituo cha muda cha wahamiaji. Picha: UNHCR

UNHCR yapongeza hatua ya kuanzishwa kwa makazi ya mpito ya wakimbizi Libya

Shirikia la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limekaribisha uamuzi wa Libya wa kuanzisha kituo cha mpito kwa ajili ya wahamiaji huko Tripoli ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuimarisha ulinzi wa kundi hilo.

Bwana Roberto Mignone ambaye ni mwakilishi wa UNHCR Libya amesema uamuzi huo wa serikali unawatengenezea wakimibizi husuan wanawake na watoto mazingira yalio salama na pia utarahisishia juhudi za UNHCR katika mchakato wa kuwatafutia wakimbizi na wahamiaji makazi ya kudumu.

Aidha Bwana Roberto ameishukuru serikali na Italia na Muungano wa Ulaya kwa juhudi za pamoja katika kutafuta suluhu la tatizo uhifadi wa wakimbizi walioko Libya.

Pia amesema UNHCR itaendelea na mikakati ya kuwatafutia makazi ya kudumu wakimbizi wapatao 40,000  .

UNHCR imesema tayari imewapatia wakimbizi 10,500 nchi ya tatu kwa ajili ya makazi ya kudumu, ila  wanasubiri taratibu za kimiundumbinu ili waweze kusafirishwa.