Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikopo bado changamoto kwa wanawake Tanzania- Matinde

Nchini Tanzania harakati zinaendelea ili kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijasiriamali na hivyo kujinasua kutoka katika lindi la umaskini. (Picha:Benki ya Dunia-Tanzania)

Mikopo bado changamoto kwa wanawake Tanzania- Matinde

Upatikanaji wa mikopo ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa sekta binafsi na mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika. Hata hivyo, utafiti uliofanyika nchini Kenya umeonyesha kwamba akiba hazikukua kwa kasi iliyotakiwa ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo kwa wafanya biashara. Aidha, utoaji mikopo ya benki binafsi hauridhishi mahitaji ya sekta binafsi. Wafanyabiashara wanazidi kutumia mbinu mbadala ya kupata mikopo, mfano kutumia mpesa ama upatu. Je harakati zikoje nchini Tanzania, Priscilla Lecomte wa Tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa  Afrika, ECA, amezungumza na Anna Matinde kutoka Tanzania na anaanza kwa kujitambulisha.