Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zilizochangwa na ushirika wa Kusini-Kusini kupambana na umasikini na njaa

Tamasha la Kusini-Kusini linaendelea Antalya Uturuki. Picha na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Ushirika wa Kusini-Kusini.

Fedha zilizochangwa na ushirika wa Kusini-Kusini kupambana na umasikini na njaa

Dola milioni 33 zilizotolewa na viongozi watatu kutoka ushirika wa Kuisni-Kusini kuzisaidia nchi 15 zenye maendeleo duni duniani kupiga hatua ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.

Hayo yamejitokeza katika ripoti ya wakfu wa IBSA iliyozinduliwa leo na India, Brazil na Afrika Kusini huko Antalya nchini Uturuki kwenye tamasha la kimataifa la ushirika wa Kusini-kusini ili kuonyesha mfano wa ushirikiano miongoni mwa mataifa yanayoendelea na mfumo wa Umoja wa Mataifa kwa faida ya mataifa mengine ya Kusini yanayohitaji msaada. Akizungumzia kuhusu usaidizi huo balozi wa Afrika Kusini nchini Uturuki Pule Isaac Malefane amesema

 (BALOZI MALEFANE CUT)

“Tuna miradi bunifu Afrika, Amerika ya Kusini , na Mashariki ya Kati , na hadi sasa fedha zimekuwa zikitumika vyema na tunatumai kwamba siku za usoni tutaweza kuongeza mara mbili msaada tunaotoa .”

 Wakfu wa IBSA ambao fedha zake zinasimamiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya ushirika wa Kusini-Kusini ulianzishwa mwaka 2004 na tangu wakati huo umekuwa ukisaidia miradi kupitia ubiya na serikali na taasisi , miradi hiyo ikijumuisha kuchagiza uhakika wa chakula, kupambana na HIV na ukimwi , hadi upatikanaji wa huduma za maji salama ya kunywa, miradi ya afya na hata kutokomeza njaa.

Katika tamasha hilo IBSA imetoa wito wa juhudi za pamoja kutokomeza umasikini na njaa katika ukanda mzima wa Kuisni