Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yapigia chepuo elimu ya kilimo cha chakula

Samaki yakaushwa nchini Cote d'Ivoire. FAO linafanya kila liwezalo ili kupunguza kupoteza kwa chakula katika sekta ya uvuvi Afrika Magharibi. Picha: FAO

FAO yapigia chepuo elimu ya kilimo cha chakula

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani Jose Graziano da Silva amesema elimu juu ya kilimo cha mazao ya chakula ndio njia mpya inayopaswa kufuatwa na nchi zote duniani katika kujihakikisha uwepo wa chakula cha kutosha na kitakachopatikana kwa uendelevu.

Bwana Graziano da Silva ameyasema hayo katika mkutano wa viongozi waandamizi wa shirika hilo huko mjini London, Uingereza.

Ameeleza uzalishaji chakula wa kutumia mbinu za kisasa unaoendelea maeneo mengi duniani kuwa na athari nyingi za kimazingira ikiwemo matumizi makubwa ya kemikali na ukataji miti hovyo umekuwa hauna usawa.

Amesema hali hiyo ndio chanzo cha watu zaidi ya watu bilioni 2 duniani kukabiliwa na ongezeko la uzito, milioni 500 wakiwa na tatizo la utipwatipwa huku wengine zaidi ya milioni 800 wakiwa na upungufu wa chakula .

Bwana Graziano da Silva amewaasa watunga sheria kuangalia ripoti mpya  iliyotolewa hivi karibuni na FAO inayoonyesha mabadiliko yanayotakiwa kufanywa ili kujihakikishia chakula kwa wananchi wao kwa kizazi cha sasa na kijacho huku zikishirikiana na nchi nyingine kwenye kutafuta dawa za kuuwa wadudu na kuzingatia sheria nyingine za chakula.