Mugabe ameondoka sasa ondoeni vikwazo Zimbabwe:UM

27 Novemba 2017

Wataalamu wawili huru wa Umoja wa mataifa wa masuala ya haki za binadamu wamekaribisha hatua ya kutomwaga damu Zimbamwe wakati wa kuhamisha madaraka kutoka kwa Rais Robert Mugabe ,na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono hatua hiyo kwa kuondoa vikwazo. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kujiuzulu kwa Mugabe kunafungua ukurasa mpya ambao ni lazima uzingatie misingi ya demokrasia na utawala wa sheria wamesema wataalamu hao anayehusika na demokrasia na anayehusika na vikwazo.

Hata hivyo wamesisitiza kuwa hilo haliwezi kufanikiwa wakati nchi hiyo ikiendelea kughubikwa na kivuli cha kiuchumi kutokana na vikwazo vya muda mrefu ambavyo kwa kiasi kikubwa vinawaathiri raia wa kawaida na kudidimiza haki za binadamu  badala ya kuleta mabadiliko ya kisiasa.

Hivyo wamesema  sasa ni wakati wa kuanza majadiliano ya kiasa nchini humo na kukarabati uchumi wa taiafa hilo huku wakiichagiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi na serikali mpya ya Zimbabwe kufufua uchumi na mifumo ya fedha na  kuweka mazingira yanayohitajkika kwa ajili ya uchaguzi huru na wa haki utakaoleta amani na mustakhbali bora nchini Zimbabwe.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud