Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto mkoani Mwanza Tanzania wapazia haki zao

Mmoja wa watoto watangazaji kwenye mtandao wa watoto wanahabari mkoani Mwanza, nchini Tanzania. (Picha: Kwa hisani ya MYCN)

Watoto mkoani Mwanza Tanzania wapazia haki zao

Leo Alhamisi tunakuletea jarida maalum likiangazia siku ya watoto duniani iliyoadhimishwa tarehe 20 mwezi huu wa Novemba. Msingi wa siku hii ni mkataba wa haki za mtoto uliopitishwa miaka 28 iliyopita ukiweka bayana haki kuu nne za msingi ambazo ni Kuishi, Kuendelezwa, Kulindwa na Kushirikishwa. Umoja wa Mataifa unataka haki hizi kuu nne zizingatiwe ili mtoto aweze kushika hatamu ya maisha yake na kwa ustawi sio wa kwake tu bali pia jamii na taifa lake. Leo basi tunakwenda Tanzania ambako tunaangazia watoto wanasemaje na mtangazaji wetu ni Getrude Clement, kutoka mtandao wa watoto mkoani Mwanza.