Utokomezaji ukatili kwa wanawake sio jukumu la wanawake pekee bali jamii nzima: UM

24 Novemba 2017

Vita ya kupinga  ukatili dhidi ya wanawake katika mifumo yote ni moja vipaumbele katika  ajenda ya Umoja wa mataifa ya  maendeleo ya mwaka 2030.

Juma hili likiwa ni la maadhimisho ya siku yakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake duniani itakayofikia kilele chake kesho  tarhe 25 Novemba ,  mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa pamoja na asasi za kiraia walijumuika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa new York Marekani kuunga mkono agenda vita hivyo.

Patrick Newman wa Idhaa hii alifuatilia kwa makini maadhimisho hayo yaliyoambatana na burudani kutoka kwa msanii Carey Muligan na ujumbe mzito na kutuandalia Makala hii ungana naye...