Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatoa wa utulivu baada ya wakimbizi kuondolewa kwa shuruti Manus

Kituo cha usaili cha wakimbizi na waomba hifadhi cha kisiwani Manus. Picha na UNHCR

UNHCR yatoa wa utulivu baada ya wakimbizi kuondolewa kwa shuruti Manus

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na ripoti kwamba nguvu imetumika kuwaondoa wakimbizi na waomba hifadhi kutoka kwenye kituo cha zamani cha usaili kisiwani Manus.

Ingawa shirika hilo limehakikishiwa kwamba hakujatumika nguvu kupita kiasi lakini limesema haliwezi kuthibitisha hilo kwani wafanyakazi wake hawajapewa fursa kamili ya kufanya tathimini kwenye kituo hicho.

Kamisha msaidizi wa UNHCR kwa ajili ya ulinzi kwa wakimbizi Volker Turk ameikumbusha serikali ya Australia kuhusu wajibu wake wa kubeba jukumu na kutoa ulinzi , usalama na suluhu ya kudumua kwa wakimbizi na waoomba hifadhi wote kwa ushirikiano na mamlaka ya Papua New Guinea .

Amezitaka serikali zote kushiriki katika mazungumzo ya kupunguza mvutano na kusaka suluhu ya muda mrefu haraka kumaliza adha hii.

UNHCR inasema timu yake kisiwani Manus inaendelea kukusanya ukweli na kupata taarifa za idadi kamili ya wakimbizi na waomba hifadhi waliosalia katika kituo hicho na maeneo mengine walikohamishiwa.

Pia inawasiliana na mashirika mengine ya kibinadamu ili kuhakikisha huduma za afya zinaweza kutolewa kwa yeyote aliyejeruhiwa.