Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nishati ni uti wa mgongo wa maendeleo ya LDC’s:UNCTAD

Nishati imeelezwa kuwa ni uti wa mgongo wa maendeleo duniani lakini nchi masikini kabisa zina upungufu mara sita zaidi ya mataifa yaliyoendelea. Picha: UNCTAD

Nishati ni uti wa mgongo wa maendeleo ya LDC’s:UNCTAD

Nishati imeelezwa kuwa ni uti wa mgongo wa maendeleo duniani lakini nchi masikini kabisa zina upungufu mara sita zaidi ya mataifa yaliyoendelea linapokuja suala la rasilimali hiyo muhimu umeonya leo Umoja wa Mataifa.

Katika ripoti yake kuhusu mataifa 47 yenye maendeleo duni au (LDC), kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD  iliyotolewa leo imesema ni mataifa manne tu kati ya hayo 47 ndio yako mbioni kufikia malengo yaliyokubaliwa kimataifa kuhusu usambazaji wa nishati ifikapo 2030.

Hata hivyo kwa mujibu wa Paul Akiwumi afisa wa UNCTAD miradi iliyoanzishwa ya nishati mbadala inayofadhiliwa na sekta binafsi imekuwa ikisaidia katika miundombinu ambayo mara nyingi imekuwa vigumu kwa serikali kuiunga mkono.

(AKIWUMI CUT 1)

“Moja ya mambo makubwa tuliyobaini ni kwamba katika nchi zenye maendeleo duni hakuna fursa kubwa ya nishati na hili linaathari kubwa kwa sababu hii inamaanisha kwamba hawawezi kuendelea na hawawezi kuendeleza viwanda katika eneo hilo, hivyo ripoti hii inabainisha kwamba ili uchumi uweze kukuwa katika nchi za LDC’s moja ya vitu muhimu ni kuwa na fursa ya kupata nishati. Misaada ya maendeleo kutoka nje asilimia 1.8 tu ndio inayoingia katika masuala ya nishatina hili ni kipengele muhimu kwa sababu nishati ni uti wa mgongo wa maendeleo.”

Ameongeza kuwa ingawa tatizo la nishati ni kubwa kwa nchi za LDC’s lakini

(AKIWUMI CUT 2)

“watu wanapiga hatua ndio maana kuanzisha kwa nishati hizi mpya mbadala ni suala muhimu, kama umebaini nchi za Afrika na nchi zinazoendelea será zao za nishati zimebadilika sio tena udhibiti wa serikali bali zinafungua milango kwa sekta binafsi , na sekta binafsi zinaweza kusambaza nishati na gridi ikasimamiwa na serikali, hivyo será zinabadilika na kuzichagiza sekta binafsi, zinachagiza kupanua wigo na zinachagiza fursa ya upatikanaji wa nishati kwa wote.