Ni lazima vijana washirikishwe majadiliano ya SDGs-Rita – sehemu ya pili

22 Novemba 2017

‘Vijana wana mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endevu yaani SDGs kwa sababu ya msukumo na ubunifu wao’ hiyo ni kauli ya Rita Kimani, kijana kutoka Kenya ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya FarmDrive nchini Kenya inayosaidia kuunganisha wakulima wadogo wadogo na fursa ya mikopo bila kuhitaji dhamana.

Aidha yeye ni mmoja wa viongozi vijana wa Umoja wa Mataifa wanaosongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambapo katika mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii na katika sehemu hii ya pili anaanza kwa kulezea namna wanavyowezesha wakulima kwa kutumia teknolojia.