Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo mpya wa usalama barabani utasaidia kuokoa maisha ya mamilioni UNECE

Afisa wa usalama barabarani anachunguza mwendo wa magari. Picha: UM

Mfumo mpya wa usalama barabani utasaidia kuokoa maisha ya mamilioni UNECE

Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Ulaya UNECE, imeanzishia mfumo mpya utakao dhibiti na  kutoa taadhari ya matukio barabarani kwa watumiaji vyombo vya usafiri wakati wa majanga au ajali.

UNECE imesema mfumo huo  mpya uitwao AECS umeandaliwa kwajili ya vyombo vya usafri lengo  likiwa ni kutoa taadhari za matukio ya dharura  kama vile kwa idara ya zimamoto au mgari ya kubeba wagonjwa wakati wa  ajali au majanga mengine  na pia kutoa ramani ya eneo la tukio ikiwa ni njia moja wapo ya kuokoa maisha kwa kutumia teknolojia mpya

Mfumo wa AECS uliopitishwa na bodi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia sheria   za usafiri wa magari namba WP.29  ikiwa ni moja ya binu zinazowezesha  teknolojia mpya  katika uboreshaji wa  usalama barabarani.

Sheria  hii mpya inatarajiwa kuanza kazi mwezi Juni  mwaka 2018  kwa nchi zitakazoweza kuitumia  chini ya  kifungu cha sheria ya mkataba  wa 1958, katika kusaidia juhudi za kimataifa za kuboresha usalama barabarani.