Kubiš alaani vikali shambulio la bomu Tuz Khurmatu Iraq:

22 Novemba 2017

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani vikali shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari Jumanne mjini Tuz Khurmatu, jimbo la Salah El Din ambapo watu kadhaa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Kubiš amesema ugaidi umeshambulia tena Iraq na kusababisha vifo na majeruhi kwa watu wasio na hatia.

Ameongeza kuwa magaidi hao wanajua wameshindwa kwenye uwanja wa mapambano na ndio maana wanageukia mbinu ya kiuoga dhidi ya watu wasio na hatia.

Ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza Maisha na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi.