Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada ya dharura ya kibinadamu bado jahitajika Syria: WHO

Kituo cha matibabu nchini Syria. Picha: WHO

Misaada ya dharura ya kibinadamu bado jahitajika Syria: WHO

Shirika la Afya ulimwenguni WHO limelaani vikali  vifo vya watu 7 na wengine 42 kujeruhiwa katika mapambano yaliotokea hivi karibuni kwenye jiji la Damascus  na maeneo jirani Mashariki mwa Ghouta, huko Syria .

Kwa mujibu wa mwakilishi wa WHO Syria Bi Elizabeth Hoff hali ya usalama wa raia Ghouta ni ya mashaka kwani matukio mengine yameripotiwa mwezi huu kati ya tarehe 14 na 17 ya watu 84 kuuawa, ikiwa ni pamoja na watoto 17 na wanawake 6 na majeruhi 659.

Aidha WHO na shirikika la msalaba nyekundu nchini humo wanasema japo wanakabiliwa na tatizo la usalama na pia miundobinu kama vile umeme, maji na mafuta ya petrol, kwa zaidi ya watu laki 4, bado wanaendelea na mikakati ya uhamisho wa majeruhi na wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharuka  kwenye vituo vya afya vilivyoko katika maeneo salama.

WHO inazidi kupaza sauti kwa mashirika ya kibinadamu na wahisani kutofumbia macho hali ya kibinadamu Syria, ikisema watu bado wanahitaji usaidizi mkubwa ili kuokoa maisha yao.