Vijana wakutana Kampala kujadili amani na usalama- WFUNA

22 Novemba 2017

Hii leo huko Kampala Uganda, kunafanyika kongamano la kimataifa la vijana liilloandaliwa na shirikisho la kimataifa la jumuiya za Umoja wa mataifa, WFUNA.

Kongamano hilo la siku mbili linajadili changamoto na pia fursa katika ujenzi wa jamii  zao kwa kuzingatia amani na usalama.

Wakati wa kongamano hilo washiriki watapata fursa za kujadili jinsi changamoto za amani na usalama  zinavyoathiri  jamii zao katika ulimwengu wa leo, katika  ngazi za kitaifa na za kikanda  kwa kutumia vipengele vya azimo  namba 2250 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,

Pia watapata nafasi ya  kujadili   masuala ya usawa wa kijinsia , unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ikiwa ni mipango ya utekelezaji wa azimio hilo.

Kongamano hili lenye lengo la kuwawezesha vijana kutoka mataifa mbalimbali kupata fursa ya kujifunza na kubadilisha mitazamo kuhusu suluhisho katika migogoro , litafika tamati kwa hotuba kutoka kwa Kessy Martine Ekomo-Soihnet ambaye ni mshauri wa vijana  kitengo cha amani na usalama.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud