Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi sio hiyari ni lazima:Guterres

21 Novemba 2017

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hatua za kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi sio starehe wala hiyari ni dharura ya lazima inayohitaji utashi wa kila mtu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hatua za kimataifa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi sio starehe wala hiyari ni dharura ya lazima inayohitaji utashi wa kila mtu.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa ngazi ya juu wa uchagizaji wa ahadi za msaada wa ujenzi mpya na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi za Caribbean (CARICOM) zilizoathirika na vimbunga Irma na Maria

Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, Guterres amezipongeza serikali za Caribbean kwa juhudi zao katika kukabiliana na vimbunga hivyo, kusaidia waathirika, kuonyesha mshikamano wa kikanda na kwa kuitisha mkutano huu.

Hasara iliyosababishwa na vingunga Irma na Maria ukiacha kupotea kwa maisha ya watu ni uharibifu wa dola bilioni 1.1 na hasara za kiuchumi zinazofikia dola milioni 400. Hivyo amesisitiza

(GUTERRES CUT)

“Nchi za Caribbean zinahitaji msaada sasa kwa ajili ya ujenzi mpya na kuchukua hatua madhubuti dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Tunahitaji kizazi kipya cha miundombinu ambayo iko tayari kwa hatari, kuweka mnepo wa kiuchumi, jamii na maisha. Kama ilivyoainisha kwenye mkataba wa Sendai wa upunguzaji hatari ya majanga , tunahitaji kuondokana na mfumo wa kudhibiti majanga na kuingia mfumo wa kudhibiti hatari.”

Ameongeza kuwa ili kufikia ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu , uwekezaji katika nyanja hizo unahitajika.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter