Tushughulikie vishawishi vya usafirishaji haramu wa binadamu- Guterres

21 Novemba 2017

Usafirishaji haramu wa binadamu hasa kwenye maeneo ya mizozo unaendelea kuwa mwiba kwa raia wasio na hatia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayo katika hotuba yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana leo kwenye mjadala wa wazi kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu.

Guterres amesema ukatili unaofanywa na wasafirishaji haramu umevuka mipaka ukisababisha machungu ya kudumu na hata vifo.

(Sauti ya Guterres)

“Ukatili wao haufahamu mipaka, ukatili wa kingono, utumikishwaji, uondoaji wa viungo vya mwili na utumwa zote ni mbinu za biashara zao.”

Ametolea mfano huko Libya ambako ripoti za hivi karibuni zimeonyesha wahamiaji wa kiafrika wakiuzwa kama bidhaa akisema..

(Sauti ya Guterres)

“Ni wajibu wetu sote kukomesha uhalifu huu. Tufikishe watekelezaji mbele ya sheria na pia tuongeze misaada ya kibinadamu.”

image
Wakimbizi nchini Libya wakiwa katika harakati za kusaka maji. (Picha:IOM-Libya)

Na zaidi ya yote Katibu Mkuu amesema..(Sauti ya Guterres)

“Lakini kuna udharura pia wa kuweka fursa zaidi za uhamiaji  halali, kurejesha maadili ya mfumo wa ulinzi wa wakimbizi, na kuongeza idadi ya wakimbizi wanaopatiwa hifadhi kwenye nchi zilizoendelea.”

Bwana GUterres amewapatia wajumbe hao ripoti yake ya utekelezaji wa azimio namba 2331 ambayo pamoja na mambo mengine inaonyesha takwimu na mbinu za kuchukua kukabili usafirishaji wa haramu.

(Sauti ya Guterres)

“Uelewa bora wa masoko na njia za usafirishaji haramu wa binadamu utaimarisha uchambuzi na uzuiaji wa vitendo hivyo.”

Na zaidi ya yote..

(Sauti ya Guterres)

“Usafirishaji haramu ni pia suala la maendeleo. Kuzuia mazingira yanayosababisha watu kutumbukia kwenye mtego, yamaanisha kukabili umaskini na kuengua watu kwa mujibu wa ajenda ya 2030 na maendeleo endelevu.”

Kwa upande wa serikali ambazo hatimaye hujikuta wakiwafungulia mashataka manusura wa usafirishaji haramu wa  binadamu, Katibu Mkuu amesema..

Katibu Mkuu ametoa wito.

(Sauti ya Guterres)

“Bila shaka wanapaswa kutendewa kama wahanga wa uhalifu na si kuwekwa korokoroni, kushtakiwa au kuadhibiwa kwa vitendo visivyo halali ambavyo walilazimika kuvifanya ili waweze kuishi.”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia Baraza la Usalama. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter