Mtoto wa Kike anakabiliwa na changamoto nyingi :UNFPA- Mosoti

21 Novemba 2017

Changamoto zinazomkabili mtoto wa Kike duniani ni nyingi, ikiwemo za ubaguzi, unyanyasaji wa kijinsia,kudhulumiwa haki zake ikiwemo haki ya kukosa elimu, ukatili, na hata ndoa za utotoni.

Sasa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA imeshikia bango haki za mtoto wa Kike na linataka kila nchi, kila jamii na kila mtu ahakikishe mtoto wa Kike na haki zake analindwa.

Katika makala hii Flora Nducha wa idhaa hii anazungumza na John Mosoti mkuu wa kitengo cha masuala ya kimataifa cha UNFPA anayeanza kwa kufafanua changamoto hizo.