Takribani miaka 7 ya vita Syria, watu milioni 13 bado wanahitaji misaada- OCHA
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA imetoa ripoti kuhusu madhara na uhitaji wa misaada ikiwa ni takribani miaka 7 tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
OCHA inasema katika kipindi hicho, misaada bado inahitajika sana kwani watu milioni 13.1, ikiwa ni wanawake, watoto na wanaume wanahitaji usaidizi wa kibinadamu.
Kati yao hao, milioni 5.6 wako kwenye maeneo hatarishi kuyafikia na wanahitaji msaada wa dharura wa kuhamishwa kwa jili ya matibabu .
Aidha ripoti hiyo ya OCHA inaonyesha kuwa migogoro inayoendelea huko Syria imekuwa chanzo kikubwa cha mahitaji ya kibinadamu, na idadi ya raia katika sehemu nyingi za nchi hiyo wanaishi kaitka hali hatarishi kwa maisha yao, hivyo kuaathiri utu na ustawi wao kila siku.