Leo ni siku ya televisheni duniani, waandaa vipindi vya UM wajinasibu

21 Novemba 2017

Leo ni siku ya televisheni duniani, waandaa vipindi vya UM wajinasibu Leo ni siku ya televisheni duniani ambapo Umoja wa Mataifa unamulika ni kwa jinsi gani televisheni inatumika kuangazia masuala yanayoendelea duniani.

Mfuko wa Umoja wa Mataifa utatumia siku hii kwenye makao makuu jijini New York, Marekani kwa kuratibu kongamano litakaloleta pamoja waigizaji wa filamu, wanaharakati na waandaaji wa vipindi vya televisheni kujadili ni kwa vipi televisheni inaibua masuala hayo.

Na ni kwa muktadha huo huo waandaaji wa vipindi vya televisheni vya Umoja wa Mataifa huweka rehani maisha yao ili kuweza kupata habari za kina kutoka maeneo hatarishi zaidi duniani ambako chombo hicho kinasaka kulinda amani. Miongoni mwa maeneo hayo ni Kidal, nchini Mali ambako ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utuvuli, MINUSMA unatekeleza wajibu wake.

Mwandaaji wa vipindi vya televisheni vya Umoja wa Mataifa Dana Fleutiaux ambaye ameshiriki kuandaa vipindi vya MINUSMA ameandika kuhusu mazingira ya kazi akisema ni magumu lakini walinda amani wanahaha kuhakikisha eneo hilo ni salama.

Akizungumzia eneo hilo la Kidal, Dana amesema ni jangwani ambako ni rahisi kuzingirwa na waasi kwa kuzingatia kuwa ni ngome ya waasi wa Tuareg. Kutokana na ulinzi wa amani, Dana ameweza kutengeneza vipindi vya kuonyesha maisha ya kila siku ya walinda amani, vipindi.