Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yapokea dola milioni 5 toka HNA, kusaidia wakimbizi Syria

Picha:WFP
Misaada ya kibinadamu ikipokelewa Syria baada ya kuwasilishwa na msafara wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na shirika la hilal nyekundu la Syria, SARC(Maktaba).

WFP yapokea dola milioni 5 toka HNA, kusaidia wakimbizi Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo  limetangaza kupokea dola milioni 5 kutoka shirika la misaada ya kibinadamu la China HNA ili kuwasaidia wakimbizi wa Syiria walioko  Uturuki,  na Lebanon kwa miaka mitatu ijayo  katika ubia mpya.

Ushirikiano huu kati ya WFP na HNA ulitiwa saini baina ya Mkurungezi mkuu wa WFP David Beasley na makamu mwenyeki wa HNA Li Xianhua mjini Beinjing China.

Bw Beasley amesema msaada huu toka HNA unazidi  kuimarisha nafasi ya  serikali ya watu wa China kwa ulimimwengu katika kutoa misaada ya kibinadamu na hususani kuhakikisha watu walioko katika mazingira magumu kama wakimbizi wa Syria wanapatia usaidizi.

Aidha Bwana Beasley ameushukuru uongonzi  mzima wa HNA kwa msaada huo ambao utatumika kusaidia katika program za  shule za watoto wakimbizi wa ndani na walioko katika maeneo tofauti huko Lebanon na Utukuri.

Ushirikiano baina ya WFP na HNA ulianza  mwaka 2013  amabapo HNA ilitoa mchango  dola milioni 1.6  ili kusaidia  chakula cha shule kwa karibu watoto 4,000 huko Ghana  na sehemu nyigine magharibi mwa Afrika.