Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yalaani daktari wake kutekwa huko Libya, yataka aachiliwe haraka

Picha@UN WHO

WHO yalaani daktari wake kutekwa huko Libya, yataka aachiliwe haraka

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limethibitisha kutekwa kwa daktari wake mmoja kutoka kituo cha afya cha Sabha kilichoko mji wa Sabha kusini mwa Libya.

Kufuatia ripoti hizo, WHO imelaani vikali kitendo hicho ikitaka wahusika wa utekaji nyara wahakikishe usalama wake na aachiliwe huru mara moja.

Katika taarifa yake WHO imesema utekaji nyara wahudumu wa afya na mashambulizi dhidi ya vituo vya afya ni kinyume na maadili na sheria na hukwamisha fursa za watu kupata huduma ya afya.

WHO imetaka pande kinzani Libya kujiepusha na mashambulizi ya vituo hivyo ambayo ni muhimu kwa ajili ya raia wanaosaka huduma.

Halikadhalika imetaka pande hizo ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu za kulinda wahudumu wa afya na vituo ambamo wanatoa huduma.