Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika:UNIDO

Siku ya maendeleo ya viwanda Afrika ambao huadhimishwa kila mwaka Novemba 20. Picha na UM/UNIDO

Viwanda ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika:UNIDO

Leo ni siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika, kauli mbiu ikiwa “Maendeleo ya viwanda Afrika ni moja ya sharti la kuwa na eneo huru la biashara yenye ufanisi na endelevu (CFTA)”.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO  lengo la siku ya mwaka huu ni kuchagiza umuhimu wa maendeleo ya viwanda Afrika katika utekelezaji wenye mafanikio ya kuwa na eneo la biashara huru na hivyo kusaidia kukuza zaidi uchumi wa bara hilo na kupiga jeki harakati za kutokomeza umasikini.

Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazingatia jukumu la ukuaji wa viwanda katika kuboresha ushindani sokoni na kuainisha hatua za muhimu zinazohitaji kuchukuliwa ili nchi za Afrika kutambua umuhimu wao.

Katika utekelezaji wa mfumo wa awamu ya pili ya muongo wa maendeleo Afrika wa (1991-2000) baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989 lilitangaza tarehe 20 Novemba kuwa ni “siku ya maendeleo ya viwanda Afrika” na tangu hapo kila mwaka mfumo wa Umoja wa Mataifa umekuwa ukiendesha matukio mabalimbali kote duniani siku hiyo kuchagiza kuhusu umuhimu wa maendeleo ya viwanda Afrika na changamoto zinazolikumba bara hilo.