Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia lazima ishikamane kudhibiti matumizi ya viuavijasumu:WHO

Kuku, WHO linasema wafugaji wasitumie Viua Vijasumu kwa mifugo wenye afya nzuri. Picha: WHO

Dunia lazima ishikamane kudhibiti matumizi ya viuavijasumu:WHO

Wiki ya kampeni dhidi ya matumizi ya viuajisasumu au antibiotic itamalizika Jumapili , huku shirika la afya Ulimwengu WHO  likitoa wito kwa nchi zote duniani kuchukua hatua kudhibiti matumizi mabaya na ya kupindukia ya dawa hizo. Flora Nducha na tarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Shirika hilo linasema matumizi mabaya na ya kupindukia ya viuavijasumu yana athari kubwa kwa afya ya binadamu na mifugo hasa baada ya dawa hizo kuwa sugu na kushindwa kutibu tena magonjwa .

Hali hiyo huchangia vifo vinavyoweza kuepukika na hasara zingine za kiuchumi , hivyo WHO imezitaka nchi kutambua hilo na kuchukua hatua za kudhibiti matumizi yake kwa kushirikiana nazo kupanga mikakati ya utekelezaji.

Dr Regina Mbindyo ni afisa wa madawa wa WHO nchini Kenya anasema wiki hii ya kampeni

(DR REGINA CUT 1)

Ameongeza kuwa kuanzia sasa WHO na  Kenya

(DR REGINA CUT 2)