Tanzania tunaelekea kulinda amani CAR na Sudan Kusini- Dkt. Mwinyi

16 Novemba 2017

Mkutano wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa umekunja huko Vancouver, Canada kwa lengo la kuangazia jinsi ya kuboresha operesheni hizo. Idadi kubwa ya operesheni ziko barani Afrika ambako mizozo na vita imegubika eneo hilo. Miongoni mwa washiriki alikuwa Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa kutoka Tanzania Dkt. Hussein Mwinyi. Kando mkutano huo Mathew Wells wa Idhaa ya Umoja wa Matafa alizungumza naye katika mahojiano haya ambayo maswali yataletwa kwako na Flora Nducha. Kwanza Dkt. Mwinyi anazungumzia Tanzania na oporesheni za ulinzi amani za Umoja wa Mataifa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud