Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neema ya maji safi kwa wanavijiji wa Buliisa nchini Uganda

Neema ya maji safi kwa wanavijiji wa Buliisa nchini Uganda

Suala la maji safi na salama ni  moja ya mambo muhimu katika ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yenye ukomo wake  mwaka 2030. Katika kufuatilia utekelezaji wa ajenda hiyo, mwandishi wetu nchini Uganda John kibego amepata fursa ya kutembelea wilaya ya Buliisa karibu na ziwa Albert nchini humo ambapo amezungumza na wenyeji  kufuatia tatizo la maji salama wanalokabiliana nao .
 
Ukosefu wa maji salama katika wilaya ya Buliza  umeathiri maisha ya baadhi ya wanavijiji  kutokana  na magonjwa kama vile  kipindupindu    na baadhi yao  kupoteza maisha   kutokana na matumizi ya maji yasiosalama .
 
Hata hivyo habari njema kwa wanavijiji katika eneo la ziwa Albert ni kwamba serikali ya Uganda kwa msaada wa mashirika ya kimataifa wamezindua mradi wa maji safi utakaosadidia  na pia kuokoa maisha ya wengi kama anavyotuhabarisha John kibego katika makala hii.