Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapopambana na ugaidi lazima tuheshimu haki za binadamu: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia mkutano kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS. Picha: SOAS, University of London

Tunapopambana na ugaidi lazima tuheshimu haki za binadamu: Guterres

Haki za binadamu bila shaka ni shememu kubwa ya suluhu ya vita dhidi ya ugaidi, amesema leo mjini London Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hotuba yake kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS.

Ameongeza kuwa"Ugaidi unashamiri wakati watu wasiokuwa na wasiwasi wanapokutana na mitazamo tofauti na kupoteza imani na mara nyingi miziz yake ni kutokuwa na matumaini na kukata tamaa na ndio sababu, haki zote za binadamu zikiwemo za kiuchumi, kijamii na kitamaduni bila shaka ni sehemu ya suluhu katika vita dhidi ya ugaidi kwani

(GUTERRES CUT 1)

“Ugaidi ni msingi wa kuzikataa na uharibifu wa haki za binadamu.

Mapambano dhidi ya ugaidi kamwe hayatafanikiwa kwa kuendeleza kuzikataa na uharibifu huo. Lazima tuendelee kupambana na ugaidi ili kulinda haki za binadamu. Na wakati huo huo, tunapolinda haki za binadamu, tunakabiliana na chanzo cha ugaidi. Kwa nguvu ya haki za binadamu kushikamana kuna nguzu kuliko nguvu za athari za ugaidi”

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres(kulia) akaribishwa kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS. Picha: SOAS, University of London
Guterres pia amependekeza mambo matano ya kuyapa kipaumbele katika vita dhidi ya ugaidi huku akisisitiza kwamba kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria kutakuwa na faida za muda mrefu. Vipaumbele hivyo ni

(GUTERRES CUT 2)

“Mosi tuahitaji ushirikiano imara wa kimataifa katika kupambana na ugaidi, pili njia ya ufanisi ya kupambana na ugaidi ni kujikita na kuuzuia, tatu kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria ni njia rahisi ya kuzuia mzunguko wa kutokuwepo utulivu na chuki. Nne ni lazima tushinde vita vya fikra. Tano na mwisho ni lazima tupazie sauti za manusura wa ugaidi.

Pia amesisitiza  kwamba ugaidi usihusishwe na dini yoyote, kabila wa rangi na kwamba hakuna sababu yoyote inayohalalisha ugaidi.

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres(kati) akaribishwa kwenye chuo kikuu cha masomo ya Mashariki na Afrika SOAS. Picha: SOAS, University of London