Serikali ya DRC yatakiwa kuheshimu haki na uhuru wa kukusanyika -Zeid
kamishina mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusitisha vitisho na hofu dhidi ya watu wanaoandamana leo kote nchi na kuitaka serikali kuhakikisha usalama wa wananchi katika misingi ya haki za binadamu chini ya sheria za kimataifa.
Baada ya serikali ya DRC kubadili tarehe ya uchaguzi mwanzoni mwa mwezi huu na kutangaza sasa uchaguzi utafanyika Desemba 2018, mashirika ya kiraia na vyama vya upinzani waliandaa maandamano ya kitaifa kupinga maamuzi ya vikosi vya usalama na wakuu wa mikoa ya Goma na Kinshasa ambapo yapiga marufuku mikusanyiko au maadamano yoyote nchini humo.
Hata hivyo kati ya tarehe 22 na 23 Oktoba, wanaharakati wa kisiasa na wa upinzani 65 walikamatwa huko Lubumbashi, kusini Mashariki mwa nchi, suala ambalo ofisi ya haki za binadamu inaendelea kupiga vita na kuitaka serikali ya DRC kuheshimu haki za binadamu .
Bwana Zeid ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa kuhakikisha wanaheshimu haki na uhuru wa kukusanyika, ushirika wa amani na uhuru wa kujieleza na pi apande zote kutumia fursa hii kueneza amani kwa jamii yote nchini humo.