Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuhamasishe sekta binafsi kudhibiti hewa chafuzi- Guterres

Mtoto kutoka Fiji akiwa na viongozi kwenye meza kuu baada ya kuhutubia mkutano wa COP23. (Picha: Video capture)

Tuhamasishe sekta binafsi kudhibiti hewa chafuzi- Guterres

Kikao cha ngazi ya juu cha mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa mabadiliko ya tabianchi, COP23 kimeanza leo huko Bonn, Ujerumani kikitoa fursa kwa viongozi wa Umoja wa Mataifa, wawakilishi wa serikali, makundi ya kiraia kupazia sauti zao mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Miongoni mwao ni mtoto kutoka kisiwa cha Fiji, waandaji wa mkutano huo akipazia sauti hatua zichukuliwe huku akikumbuka kilichowakumba..

(Nats)

Anasema mapema mwaka 2016, tulipigwa na kimbunga kikubwa kuwahi kupiga Fiji! kimbunga hiki kilikuwa kikali zaidi kuwahi kupiga eneo la kusini mwa dunia…

Nyumba yangu, shule yangu, vyanzo vya chakula, fedha! Vyote vilisambaratishwa kabisa!

Hebu na tuwe makini kwenye masuala ya mazingira na tusaidie kulinda vyema sayari mama yetu dunia!

Nats..

Na ndipo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akapanda jukwaani akisema kuwa sasa ni wakati wa kuongeza kasi na kusonga mbele tena kusonga mbele kwa haraka na kwa pamoja.

image
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia COP23. (Picha:VideoCapture)
Amesema uharibifu utokanao na madhara ya mabadilko ya tabianchi ni makubwa kupindukia. Mafuriko, mioto, vimbunga vya kupita kiasi imekuwa ni kawaida.

(Sauti ya Guterres)

“Viwango vya hewa ya ukaa kwenye anga la juu ni vya juu kuliko miaka 800,000 iliyopita. Mabadiliko ya tabianchi ndio yatakayoainisha zama zetu. Wajibu wetu kwa kila mmoja wetu na vizazi vijavyo ni kuongeza matamanio yetu katika mambo makuu matano. Utoaji wa hewa chafuzi, kukabili madhara, fedha, ubia na uongozi.”

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesema..

(Sauti ya Guterres)

“Njia pekee ya kuhakikisha kiwango cha hewa chafuzi kinaendelea kuwa chini ya nyuzi joto 2 na ikiwezekana nyuzijoto 1.5 ni kuhamasisha sekta binafsi kufanya marekebisho ya matumizi ya nishati. Kukiwa na vihamasisho vya serikali kama vile sera bora za matumizi ya nishati salama na sera za usafirishaji, sekta ya biashara inaweza kusongesha masoko kwa kuendeleza uchumi tunaohitaji unaohitaji mazingira.”