Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA itafanikiwa nchini Mali ikiwezeshwa: Deconinck

Kamanda mkuu wa vikosi vya MINUSMA nchini Mali , Meja Jenerali Jean-Paul Deconnick. Picha na UM/ Matthiew Wells

MINUSMA itafanikiwa nchini Mali ikiwezeshwa: Deconinck

Kamanda mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali (MINUSMA) ulioghubikwa na madhila ikiwemo idadi kubwa ya vifo, upungufu wa vifaa na wafanyakazi ameahidi kufanikiwa endapo atapatiwa nyenzo zinazohitajika katika kazi yake.

Kamanda huyo wa (MINUSMA), Meja Jenerali Jean-Paul Deconinck, ameyasema hayo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mawaziri wa ulinzi mjini Vancouver, Canada alipokuwa akitoa taarifa kwa mawaziri na maafisa wa jeshi kwenye kikao kuhusu kuusaidia mpango wa MINUSMA ambako zaidi ya walinda amani 30 wa Umoja wa Mataifa wameuawa mwaka huu kufuatia mashambulizi yenye itikadi kali.

Akizungumza na UN News kandoni mwa mkutano huo kamanda Deconinck ameeleza ni kwa nini anahudhuria mkutano huo.

(DECONNICK CUT)

“Kutoa taarifa ya nini nahitaji kama kamanda wa MINUSMA , ili kufanikiwa katika mpango wangu , kwa sababu kuna mapengo , katika kukabiliana na vitisho, kupunguza hatari, na wakati huohuo kulinda watu wangu , kulinda jamii na kutekeleza majukumu yangu “