Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Tanzania hadi Sudan Kusini kusaidia ulinzi wa raia- Meja Paschal

Meja Raphael Paschal, mchambuzi wa taarifa za wakimbizi wa ndani, UNMISS. (Picha:UNMISS)

Kutoka Tanzania hadi Sudan Kusini kusaidia ulinzi wa raia- Meja Paschal

Maafisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania, JWTZ ni miongoni mwa watendaji katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan  Kusini, UNMISS. Maafisa hao wana majukumu mbalimbali yote yakichangia kufanikisha ulinzi wa raia na amani kwenye taifa hilo change zaidi duniani ambalo sasa limegubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwezi disemba mwaka 2013. Je ni yapi miongoni mwa majukumu hayo? Daniel Dickinson, ambaye ni msemaji wa UNMISS amefanikisha mahojiano na mmoja wa maafisa hao naye si mwingine ni Meja Raphael Paschal, mchambuzi wa taarifa za wakimbizi wa ndani, UNMISS. Assumpta Massoi amekamilisha mahojiano hayo na Meja Paschal anayeanza kwa kuelezea kile anachofanya.