Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali Yemen yaendelea kudorora-UNHCR

Watoto nchini Yemen, maisha yao yako hatarini kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo. (Picha:OCHA/G.Clarke_Maktaba)

Hali Yemen yaendelea kudorora-UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea kusikitishwa kwake na hali inayoendelea kudorora Yemen kufuatia kuendelea kufungwa kwa mipaka ya kuingia nchi hiyo kupitia ardhi, bahari na anga tangu tarehe 6 mwezi huu.

Kwa kipindi cha wiki moja kufungwa kwa mipaka kumezuia kuwasilishwa kwa misaada ya kibinadamu na bidhaa za mauzo na  pia kudhibiti safari za watoa huduma.

UNHCR imesema hali hiyo naleta matatizo ya kiuchumi kwa wakazi ambao tayari wanakabiliwa na madhila ya miezi mingi ya mzozo.

Mzozo wa Yemen ambao ulianza Machi 2015 umesababisha janga kubwa zaidi la kibinadamu huku watu milioni 21 wakiathirika.

Wakati hali inaendelea kuwa mbaya watu wamekata tamaa na wanageukia mbinu hatari kama vile ajira kwa watoto, utumikishwaji na ndoa za mapema.