Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid kuanza ziara El Salvador tarehe 15 mwezi huu

Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’aad al-Hussein. UN/Jean-Marc Ferré

Zeid kuanza ziara El Salvador tarehe 15 mwezi huu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid zaRa'ad Al Hussein  atatembelea El Salvador kwa mwaliko wa serikali kuanzia tarehe 15 hadi 16 mwezi huu ili kujadili maendeleo na changamoto zinazohusu haki za binadamu nchini humo.

Bwana Zeid ambaye atakuwa Kamishna Mkuu wa kwanza wa haki za binadamu kutembelea El Salvador, atakutana na Rais Salvador Sánchez Cerén.

Pia atakutana na viongozi wengine waandamizi akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa sheria na Usalama wa Umma, wanachama wa tume za haki za binadamu, Mwanasheria Mkuu wa serikali,  na rais wa tume ya mambo ya nje ya bunge la sheria .

Katika ziara hiyo Bwana Zeid atatakutana pia na  wawakilishi wa vyama vya kiraia , wanaharakati  wa haki za binadamu, na pia atatembelea maabusu ya wanawake.