Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanamke ana mchango mkubwa katika utunzaji wa mazingira:COP23

Mwanamke ana mchango mkubwa katika utunzaji wa mazingira:COP23

Wakati mkutano wa 23 wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa, COP 23, ukiingia wiki ya mwisho ya majadiliano mjini Bonn, Ujerumani, Rais wa mkutano huo leo jumapili ametangaza mpango wa utekelezaji wa kijinsia kwa kutambua nafasi ya wanawake katika suala la mabadiliko ya tabianchi

Akizungumza na waandishi wa habari Frank Bainimarama, ambaye pia ni waziri mkuu wa Fiji, amesema washirika wote kweye kikao cha ngazi ya juu walifikia uamuzi wa kutambua nafasi ya wanawake katika utunzaji wa mazingira.

Naye mkurugenzi mtendaji wa COP23 Nazhat Shameen Khan akichangia hoja hiyo amesema ujumuishwaji wa   jinsia  zote katika kukabiliana na mbadiliko ya tabianchi kitaifa na kimataifa ni sera muhimu sana.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres pamoja na viongozi  mbalimbali wa serikali na asasi za kiraia wanatarajiwa kukutana katika kikao cha ngazi ya juu kwenye mkutano huo wa COP23, tarehe 15 na 16 Novemba ili kujadili utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi katika ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030..