Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia wakimbizi kurejea nyumbani CAR

IOM yasaidia wakimbizi kurejea nyumbani CAR

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limekamilisha shughuli ya kuhamisha wakimbizi wa ndani 698 kutoka kambi ya muda karibu na kituo cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR, MINUSCA waliochukua hifadhi kufuatia mashambulizi ya 2016 mji wa Kaga Bandoro.

Zaidi ya wakimbizi 20,000 kutoka CAR waliwasili karibu na kituo hicho baada ya kikundi cha wapiganaji wa zamani wa Seleka kushambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Evêché.

Hali ya hatari ya wakimbizi hao imesababisha IOM na watoa huduma nchini CAR kufikia uamuzi wa kuhamisha wakimbizi waliokuwa wanakabiliwa na hatari ya kiafya na hali ngumu ya kutua kwa ndege kwenye eneo hilo ambako kulihatarisha shughuli za kibinadamu.

IOM imesaidia familia hizo kwa usafirishaji wa mali yao na kuwapatia pesa taslimu kila kaya na bidhaa za kujikimu.

CAR inakabiliwa na kuzuka tena kwa ukatili na kuna hatari ya hali ya miaka mine iliyopita kujitokeza tena.