Jarida la leo kwenye YOUTUBE #SUBSCRIBE

9 Novemba 2017

Sasa waweza pia pata jarida letu kupitia Youtube @UNNewsKiswahili. Katika ukurasa wetu wa Youtube utapata Jarida la kila siku bila kusahau habari za adhuhuri ambazo hatukuweza kukuletea kwenye jarida la asubuhi. Halikadhalika video ya Wiki Hii. SUBSCRIBE ili upate habari kila wakati kutoka Umoja wa Mataifa. Leo tumeangazia kitendo cha nchi kuendelea kuagiza vyakula kutoka nje ya nchi zao licha ya uzalishaji wa chakula kuongezeka. halikadhalika tunaangazia ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID kuangazia ulinzi thabiti wa amani. Makala inakwenda Kagera nchini Tanzania, afya kwa wazee bila kusahau tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.