Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya afya kwa wazee yaleta nuru Tanzania

Huduma ya afya kwa wazee yaleta nuru Tanzania

Upatikanaji wa huduma ya afya ni changamoto katika jamii nyingi na hali inakuwa mbaya zaidi kwa wazee kwani mara nyingi licha ya uwepo wa sera, mara kwa mara kundi hili linakabiliwa na ubaguzi.

Katika Makala hii tunaelekea mkoani Kagera nchini Tanzania tukiangazia uboreshaji wa huduma ya afya kwa wazee, moja ya kipengele cha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambapo Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM kutoka Kagera, Tanzania ameangazia kundi hilo ambalo sasa hivi kuna nuru gizani kufuatia serikali kutoa vitambulisho ili kupata bima ya afya.