China yaipatia WFP fedha kusaidia wakimbizi Niger

9 Novemba 2017

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha msaada wa dola milioni 1 kutoka serikali China katika kuchangia shughuli za dharura shirika hilo.

Fedha hizo zinalenga kupunguza mateso ya wakimbizi wa ndani na wahamiaji katika eneo la Diffa huko Niger.

Sory Ouane ambaye ni mkurugenzi wa WFP Niger amesema fedha hizo zitasaidia juhudi za kuimarisha hali ya lishe ya watoto zaidi ya 16,000 wenye umri wa chini ya miaka miwili.

Amesema, zaidi ya watoto wanne kati ya kumi wameathirika na utapiamlo sugu ambapo kiwango hicho ni sawa na asilimia na 17.5 ya watoto katika eneo la Diffa.

Aidha amesema mchango huu pia utasaidia mahitaji ya chakula kwa watu wazima na wanawake wajawazito zaidi ya 200,000 huko Diffa .

WFP inawahimiza wahisani waelekeze misaada yao Niger ili kusaida wakimbizi na wahamiaji hao wanaonyanyaswa na Boko Haram.