UNAMID yatakiwa kulinda mali na wafanyakazi wa UM kwa gharama yoyote

9 Novemba 2017

Walinda Amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda Amani Darfur Sudan UNAMID, wametakliwa kuhakikisha mbali ya kulinda raia wanawalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mali za Umoja huo kwa gharama yoyote. Mwandishi wa UNAMID Luteni selemani Semunyu na ripoti kamili.

(TAARIFA YA SELEMANI)

Agizo hilo limetolewa na naibu mkuu wa majeshi ya ulinzi wa amani Sudan Kusini Meja Jenerali Fida Hussain Malik wakati wa ziara yake ya kikazi katika makao makuu ya vikosi vya Tanzania vilivyopo eneo la Khor Abeche.

Amesema kufuatia zoezi la kuwanyang’anya raia silaha kwa nguvu baada ya muda wa kusalimisha kwa hiyari kumalizika, walinda amani wanapaswa kuwa tayari kuhakikisha majengo ya Umoja wa Mataifa, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa makambini na mali vinalindwa na yeyote atakeyeshambulia wana haki ya kujihami kwa njia yoyote.

(MEJA JENERALI HUSSAIN MALIKI CUT)

Pia amepongeza jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kwa kufanya dorioa katika maeneo ya Jamer Mara Mashariki eneo ambalo sio rahisi kufikika na kuwataka kuendeleza weledi huo kitakapoanzisshwa kikosi kazi maalumu katika eneo hilo.

Naye kamanda wa sekta ya Kusini Brigedia Jenerali Godwin Umelo amesema mafanikio yaliyopatikana katika doria  iliyofanywa na Tanzania yametokana na utimamu wa askari wake uliotokana na kiwango cha mafunzo.

(BRIGEDIA JENERALI UMELO CUT)

Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha Tanzania (TANZBATT11)Kanali William Sandy wataendeleza weledi huo uliotokana na maandalizi mazuri tangu Tanzania.

(KANALI SANDY CUT)

Vikosi vya Tanzania hivi karibbuni vimefanya doria katika vijiji ambavyo havijawahi kufikiwa na vikosi vya UNAMID kwa Zaidi ya miaka 10.