Tanzania na kasi ya maendeleo endelevu SDGs: Mero

10 Novemba 2017

Tanzania inatekeleza kwa kasi ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGs kwa kuchukua hatua kadhaa ikiwemo ya awali ya kutafsiri malengo hayo kwa lugha ya Kiswahili na kuelimisha wananchi mashinani namna ya kutumia fursa zilizopo. Selina Jerobon na ripoti kamili.

(Taarifa ya Selina)

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York, Balozi Modest Mero amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii mjini humo.

Balozi Mero amesema ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma, mkakati wa kukuza uchumi wa viwanda kwa kuboresha nishati ya umeme unatiliwa mkazo huku akieleza wajibu wa ofisi yake katika kutekeleza sera hiyo.

(Sauti Balozi Mero)

Kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji ambayo hata Benki ya Dunia imesema hivi karibuni ni lazima Tanzania ichukue hatua, Balozi Mero amesema..

(Sauti Balozi Mero)