UNISFA imedhamiria kukomesha unyanyasaji na ukatili wa kingono

10 Novemba 2017

Wakati mkutano wa wiki ya polisi ukiendela hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani, afisa mshauri wa polisi kwenye mpango wa Umoja wa Mtaifa eneo la Abyei mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini UNISFA amesema, mpango huo umedhamiria kukomesha vitendo au nia ya kutekeleza unyanyasaji na ukatili wa kingono. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kandoni mwa mkutano huo anikutana na fisa huyo Bi Mary Gahonzire aliyenieleza kuwa nia kuhakikisha hakuna wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wala jamii wanayoihudumia wanajihusisha na vitendo hiyo ingawa wanachangamoto moja kubwa

(MARY CUT 1)

Hapo akimaanisha msuala ya magereza.Pia amesema pamoja na changamoto hiyo wameanza mkakati kabambe wa uelimishaji dhidi ya uhalifu huo, wakishirikisha wadau wote zikiwemo  shule, raia katika ngazi zote, familia ya Umoja wa Mataifa na familia ya UNSFA, na matunda yameanza kuonekana kwa  wanafunzi wa shule, kina mama, kina baba, wavulana na wasicha kufahamu kuhusu unyanyasaji na ukatili wa kingono kuwa ni uhalifu