Serikali ya Syria na Daesh walitumia silah za maangamizi-JIM Ripoti

7 Novemba 2017

[caption id="attachment_331311" align="aligncenter" width="625"]03hapanapalejimripoti

Kikosi kazi  cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na shirika la kupinga matumizi ya silaha za maangamizi OPCW kijulikanacho kama JIM  leo kimewasilisha ripoti yake  ya uchunguzi kuhusu matumizi ya silaha za kemikali  nchini Syria kwenye kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York  Marekani na kusema pasi shaka silaha hizo zilitumiwa na pande zote katika mzozo , jeshi la serikali ya Syria na wanamgambo wa Daesh .

Bwana Edmund Mulet, ambaye ndiye mkuu wa  JIM,akiwasilisha ripoti yake mbele ya baraza la usalama  amesema wamefanya uchunguzi wa  kina, wa kitaaluma na kisayansi katika mashambulizi ya kemikali Syria, ambapo zaidi ya watu 90 walipoteza maisha.

(MULLET CUT 1)

“Nimewasilisha hitimisho la matukio mawili tuliyochunguza mwaka huu  ikiwa ni pamoja na matumizi ya silah za kemikali huko Khan Shaykhun April 4 mwaka huu na vikosi vya Jeshi la serikali ya Syria na matumizi mengine ya  kemikali Septemba mwaka jana ambayoyalifanywa na wanamgambo wa Daesh Um Hosh.”

Aidha katika kufafanua mbinu zilizotumika kufikia hitimisho la uchunguzi huo amesema...

(MULLET CUT 2)

Tunashirikiana na  watalaamu kutoka mashirika na taasisi mbalimbali, wanasayansi, wanajeshi na pia tunazihusisha mahabara huru katika kukusanya sampuli za kemikali na silaha zilizotumika katika maeneo tofauti na kuzifanyia uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli.