Hali ya mjane kutoka Uganda ni msumari wa moto juu ya kidonda-sehemu 1

7 Novemba 2017

Wakati Umoja wa Mataifa ukichagiza nchi kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma kuelekea ukomo wa malengo ya maendelo endelevu yaani SDGs bado kuna changamoto ambazo huenda zikakwamisha ufikiaji wa malengo hayo. Wanawake na waisichana mara kwa mara wanakabiliwa na aina mbali mbali ya ubaguzi ikiwemo suala la urithi wa mali hususan katika jamii zilizoko nchi zinazoendelea.

Katika makala ifuatayo John Kibego, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili kutoka Uganda amezungumza na mjane aliyepitia madhila mengi kufuatia kifo cha mumewe, Magdalena Mbiya Namutebi alipoteza mumewe takribani miongo mitatu ilyopita na kusalia akilea watoto wanane peke yake. Kulikoni ungana nao