MINUSCA imejizatiti kusaidia CAR kupata amani

6 Novemba 2017

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili hali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu nchini CAR Parfait Onanga- Anyanga  amesema ombi la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kutaka kuongezwa kwa vikosi vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, MINUSCA ni sehemu ya mpango wa kukabiliana na hali mbaya ya kiusalama inayozidi kuzorota nchini humo.

Bwana Onanga-Anyanga akisisitiza kwamba hali ya kiusalama bado inasuasua na ile ya kibinadamu inasikitisha amesema vikosi hivyo vinatakiwa kuwa na walinda amani walio na mbinu za usafiri wa hali ya juu kwa ajili ya kuwezesha kufika kwa urahisi maeneo ambako raia wako hatarini.

Kwa mantiki hiyo amesema…

(Sauti ya Parfait)

“Ujumbe ninaojivunia kuongoza hautasita kwa namna yoyote kusaidi serikali na mamlaka Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na wadau wa kitaifa ambao wamedhamiria amani, kufikia ndoto za wananchi hususan vijana, wanawake na watoto kwa ajili ya mustakabali salama na bora.”

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa CAR katika ofisi ya Umoja wa Mataifa balozi, Ambroisine Kpongo, amesema ziara ya katibu mkuu ya hivi majuzi ilikuwa ni ya kihistoria na mfano muhimu kwa watu wa nchi hiyo amabo wameteseka sana.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter