Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chondechonde Hong Kong watendeeni haki wanaharakati wa demokrasia:UM

Chondechonde Hong Kong watendeeni haki wanaharakati wa demokrasia:UM

Jopo la watalam  wa haki za kibinadamu wa  Umoja wa  Mataifa wameiasa mamlaka ya Hong Kong kuheshimu ahadi zake katika kutekeleza haki za binadamu kwa  wanaharakati wa kidemokrasia watatu watakaokata rufaa kupinga  hukumu zao tarehe 7 Novemba.

Wanaharakati hao Joshua Wong, Nathan Law na Alex Chow walifungwa mwezi Agosti ambapo mmoja kati yao alihukumiwa kwa miezi sita na mwingine  miezi mne kutokana na nyadhifa zao  za kiungozi,  kwa sababu ya maandamano ya mwaka 2015, ambapo waliachiwa huru  kwa  dhamana  wakati wakisubiri rufaa .

Katika  taarifa ya pamoja wataalam hao wa haki za binadamu wamesema ni lazima mahakama  ya Hong Kong ifuate sheria ya kimataifa katika kuwatendea haki wahukumiwa hao na pia wametoa wito kwa mamlaka ya Hong Kong kuheshimu uhuru wa mahakama na utawala wa sheria

Aidha wataalamu hao wameitaka mamlaka ya Hong Kong kusimamia haki katika kulinda uhuru wa kujieleza na wa mikutano ya amani chini ya azimio la Kimataifa la Haki za kiraia na kisiasa, ambalo Hong Kong ni mwanachama .