Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhara ya tsunami ni makubwa licha ya uhaba wa matukio

Madhara ya tsunami ni makubwa licha ya uhaba wa matukio

Leo Novemba tano ni siku  ya kimataifa ya kuhamasisha dunia kuhusu athari za Tsunami, ikiwa ni mwaka wa pili wa maadhimisho hayo yanayolenga kupunguza idadi ya watu wanaoathiriwa na majanga kote ulimwenguni ifikapo 2030.

Visa vya tsunami licha ya kwamba havifanyiki mara kwa mara lakini vina madhara makubwa huku ikielezwa kuwa katika kipindi cha miaka mia moja iliyopita visa 58 vya tsunami vimesababisha maafa kwa zaidi ya watu 260,000 au  wastan wa watu 4,600  kwa janga ikiwa ni  idadi ya juu zaidi kuliko  janga lolote la asili.

Ukuaji wa miji wa haraka na kuimarika kwa utalii katika maeneo yaliyo hatarini kukumbwa na tsunami vina hatarisha watu wengi zaidi. Hivyo kufanya upunguzaji wa hatari kuwa mgumu.

Siku hii inaadhimishwa kwa mwaka wa pili kufuatia kupitishwa  azimio na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Desemba 2015.