Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam huru wa haki za binadamu kuchunguza unyanyasaji wa watoto nchini Laos

Mtaalam huru wa haki za binadamu kuchunguza unyanyasaji wa watoto nchini Laos

Mtaalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa atafanya ziara rasmi kkatika Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Laos kuanzia tarehe  8 hadi 16 Novemba ili kuchunguza  unyanyasaji wa watoto nchini  humo.

Bi Maud de Boer-Buquicchio, amabye ni mtaalam huru wa haki za binadamu amesema anashukuru  mwaliko wa serikali ya Laos katika jitihada za kuwasaidia kuendeleza na kulinda haki za watoto.

Amesema katika ziara yake atatathmini hatari na aina ya unyanyasaji  wa watoto , pamoja na hatua mkakati  zinazochukuliwa na Laos katika kupambana na tatizo hilo.

Aidha katika wa ziara yake ya siku tisa, Bi de Boer-Buquicchio atasafiri kwenda mji mkuu, Vientiane, na mikoa ya Oudomxay, Champasak na Salavan ambako atakuatana na watoto waathirika, maafisa wa  mahakama, mamlaka ya mkoa na serikali za mitaa, wawakilishi wa mashirika ya kibinadamu  yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi na wanachama wa jumuiya ya kimataifa.

Mwishoni mwa ziara yake, mnamo tarehe 16 Novemba Bibi-Boer-Buquicchio atakutana na waandishi wa habari k na kisha kuwasil;isha ripoti yake kwenye Umoja wa Mataifa.