Vijana kushiriki kilimo si kosa- Restless Development sehemu 2

1 Novemba 2017

Vijana vijana vijana! Umoja wa Mataifa unasema ndio muarobaini wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Na ni kwa mantiki hiyo wakati wa mikutano ya ngazi ya juu ya mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, vijana kutoka pande mbalimbali za dunia walifika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuelezea kile wanachofanya mashinani ili kusongesha ajenda ya maendeleo na wakati huo huo kukwamua maisha yao. Miongoni mwao ni vijana Rachel Proefke na RoselynMugo wa shirika la kiraia la Resteless Development kutoka Kenya ambao walizungumza na Grace Kaneiya na kumweleza shughuli zao. Katika sehemu hii ya pili Roselyn ananza kueleza ushiriki wa vijana katika kilimo