Mateso ya watoto vitani ni aibu yetu wenyewe- Guterres
Kiashirio hicho cha kutoka kwa kiongozi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Oktob, nafasi ambayo inashikiliwa na Ufaransa. Anatangaza kuanza kwa mjadala wa wazi na hivyo kila mjumbe awe sawa.
Huyu ni Waziri wa Ufaransa anayehusika na masuala ya Ulaya na mambo ya nje Jean-Yves Le Drian na ameongoza mahsusi kikao hiki kinachoangazia watoto kwenye mizozo ya kivita.
Bwana Le Drian akampatia fursa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ili aweze kuhutubia wajumbe.
Nats-2-Guterres
Bwana Guterres anawaeleza wajumbe kuwa ripoti iliyo mbele yao kuhusu watoto katika mizozo kwa mwaka 2016 inaweka bayana kuwa watoto wameendelea kuathirika kwa njia mbali mbali kutokana na uamuzi na vitendo vya viongozi wa kisiasa na kijeshi.
“Watoto duniani kote wanateseka na mizozo isiyokubalika. Hii ni chanzo cha aibu kubwa ya dunia. Kipindi husika kwenye ripoti kimeonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto. Tunashuhudia vikundi vilivyojihami vikilazimisha wasichana na wavulaka kujilipua. Watoto wananyanyapaliwa kwa kutumimishwa na vikundi vilivyojihami. Watoto wanaswekwa rumande kwa uhalifu ambao hawajafanya. Na tunashuhudia pande kinzani kwenye mizozo wakizuia misaada ya kuokoa maisha ya watoto.”
Hivyo amesema,
(Sauti ya Guterres)
“Iwapo tutaacha kizazi kijacho kwenye kiwewe na kikiugulia machungu, tunakuwa tumewasaliti wale ambao tunawahudumia na tunajisaliti wenyewe.”
(Sauti ya Virginia)
“Taarifa zetu za hivi karibuni zaidi zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaotumikishwa na kutumika imesalia ni kubwa sana huko Sudan Kusini na Somalia. Mashambulizi dhidi ya shule na hospitali bado ni mengi mno huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.”
Mathalani wajumbe wamesema wameshawishika kuwa ulinzi wa watoto kwenye mizozo unapaswa kuwa jambo muhimu katika mkakati wa kimsingi wa kutatua mizozo na kuendeleza amani.
Baada ya kuhakikisha wajumbe wameridhia taarifa hiyo ya rais, ndipo Waziri La Drian akazungumza kwa niaba ya Ufaransa akisema kuwa
(Sauti ya La Drian)
“Tunatakiwa kusonga mbele na lengo letu la kuwa na dunia bila ya watoto kwenye maeneo ya vita. Tunapaswa kuwajibika kuhakikisha kuwa watoto wanakuwepo maeneo ambayo wanapaswa kuwepo. Mathalani shuleni na katika familia zao pendwa na badala ya kuwa kwenye maeneo ya vita. Huu ni wajibu wetu wa kimataifa.