Ubunifu Burundi wahakikisha hedhi salama kwa wasichana
Idadi kubwa ya wasichana na wanawake nchini Burundi wana matatizo ya utumiaji taulo za kike au sodo. Asilimia kubwa kutokana na ukosefu wa pesa wanatumia nguo, huku wengine wakitumia majani na hivyo kuwasababishia athari kubwa za kiafya . Shirika moja la vijana nchini humo la SACODE (SAKODE) baada ya kutafakari kero hiyo liliamua kutengeneza taulo za kike au sodo kwa vifaa vya nyumbani na kuipanga bei kuzingatia hali ya kipato cha wanawake nchini Burundi.Wasichana wengi shuleni wamenufaika kwa kupewa taulo hizo za kike bila malipo. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu , Ramadhani KIBUGA amefuatilia hali hiyo na ametuandalia makala hii kutoka mjini Bujumbura, Burundi.