Maelfu ya raia wa Cameroon wakimbilia nchini Nigeria

31 Oktoba 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR, pamoja na mamlaka ya  Kusini Mashariki mwa Nigeria, wamepokea maelfu  ya wakimbizi kutoka Cameroon waliokimbilia  nchini humo kutafuta hifadhi na usalama, baada ya uhasama mpya uliozuka mwezi oktoba katika eneo linazumgumza kiingereza  Cameroon.

UNHCR na tume ya taifa ya Wakimbizi (NCFRMI)  wanasema hadi sasa wameandikisha wakimbizi 2,000 kwa msaada wa wananchi wa eneo hilo la kusini Mashariki mwa Nigeria. Wamesema wakimbizi wengine  zaidi wanasubiri usajili, na wengi  bado wapo mafichoni katika misitu ya Camerron wakati wanajaribu kuvuka mpaka.

Aidha UNHCR na serikali ya Nigeria wamesema wapo katika mchakato wa kuaanda eneo jipya la kuwahifadhi wakimbizi hao. Pia wametoa misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na magodoro, mablanketi, vyandarua, vifaa vya kupikia na kujisafi, na tani 40 za chakula.

UNHCR imesema itaendelea kushirikiana na serikali ya  Nigeria na mashirika ya kibinadamu katika kutoa huduma kwa wakimbizi hao, wakiwa na hofu   kwamba idadi ya wakimbizi hao inaweza kuongezeka kufikia  40,000 kutokana la taarifa kutoka mashinani  ambako migogoro inaendelea.

Nigeria na Cameroon tayari wanakabiliwa na janga la boko Haramu katika eneo la Ziwa Chad ambalo tayari limewaathriri watu zaidi milion 2.5

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter